Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Luka 1:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu, jina lake ni takatifu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu, jina lake ni takatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu, jina lake ni takatifu. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana yeye Mwenye Nguvu amenitendea mambo ya ajabu: jina lake ni takatifu. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana yeye Mwenye Nguvu amenitendea mambo ya ajabu: jina lake ni takatifu. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. |
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Kwa hiyo, asema Bwana, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitalipiza kisasi kwa adui zangu;
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.
Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likateremka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapatao elfu mbili; wakafa baharini.
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.