Kutoka 8:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akafanya; wakaja inzi wengi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa na wale inzi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akafanya kama alivyosema: Makundi makubwa ya nzi yakaivamia nyumba ya Farao, nyumba za maofisa wake na nchi nzima ya Misri. Nchi nzima ya Misri ikaharibiwa na nzi hao. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akafanya kama alivyosema: Makundi makubwa ya nzi yakaivamia nyumba ya Farao, nyumba za maofisa wake na nchi nzima ya Misri. Nchi nzima ya Misri ikaharibiwa na nzi hao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akafanya kama alivyosema: makundi makubwa ya nzi yakaivamia nyumba ya Farao, nyumba za maofisa wake na nchi nzima ya Misri. Nchi nzima ya Misri ikaharibiwa na nzi hao. Neno: Bibilia Takatifu Naye Mwenyezi Mungu akafanya hivyo. Makundi makubwa ya inzi walimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na inzi. Neno: Maandiko Matakatifu Naye bwana akafanya hivyo. Makundi makubwa ya mainzi yalimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na mainzi. BIBLIA KISWAHILI BWANA akafanya; wakaja inzi wengi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa na wale inzi. |
Au kwamba huwapi ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta inzi wengi sana juu yako wewe, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na nyumba za Wamisri zitajawa na inzi wengi sana, na nchi nayo ambayo wa juu yake.
Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.