Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakarukaruka juu ya madhabahu waliyoifanya.
Kutoka 8:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakawakusanya marundo marundo; na nchi ikatoa uvundo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wakawakusanya vyura hao marundo marundo; nchi nzima ikanuka. Biblia Habari Njema - BHND Watu wakawakusanya vyura hao marundo marundo; nchi nzima ikanuka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wakawakusanya vyura hao marundo marundo; nchi nzima ikanuka. Neno: Bibilia Takatifu Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. Neno: Maandiko Matakatifu Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. BIBLIA KISWAHILI Wakawakusanya marundo marundo; na nchi ikatoa uvundo. |
Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakarukaruka juu ya madhabahu waliyoifanya.
Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeangalia.
Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote ya Misri.
BWANA akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba.
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
BWANA akafanya; wakaja inzi wengi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa na wale inzi.
Nao wale waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya hayo majipu, kwa maana hao waganga walikuwa na majipu, na Wamisri wote walikuwa nayo.
Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?
Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa.