Kutoka 7:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa na Haruni wakafanya vivyo hivyo; kama BWANA alivyowaambia, ndivyo walivyofanya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose na Aroni wakafanya hivyo; naam, walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose na Aroni wakafanya hivyo; naam, walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose na Aroni wakafanya hivyo; naam, walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Neno: Bibilia Takatifu Musa na Haruni wakafanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaamuru. Neno: Maandiko Matakatifu Musa na Haruni wakafanya sawasawa kama vile bwana alivyowaagiza. BIBLIA KISWAHILI Musa na Haruni wakafanya vivyo hivyo; kama BWANA alivyowaambia, ndivyo walivyofanya. |
Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo hivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
Utanena hayo yote nikuagizayo; na ndugu yako Haruni atanena na Farao, ili awape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.
Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.