Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Kutoka 6:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amramu alimwoa Yokebedi, shangazi yake, naye akamzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. Biblia Habari Njema - BHND Amramu alimwoa Yokebedi, shangazi yake, naye akamzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amramu alimwoa Yokebedi, shangazi yake, naye akamzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. Neno: Bibilia Takatifu Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, aliyemzalia Haruni na Musa. Amramu aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). Neno: Maandiko Matakatifu Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Haruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137. BIBLIA KISWAHILI Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. |
Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu.
Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao.
Basi vizazi vya Haruni na Musa, siku hiyo BWANA aliyosema na Musa katika mlima wa Sinai, ni hivi.
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.