Kutoka 6:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa yafuata majina ya wana wa Lawi na wazawa wao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. Biblia Habari Njema - BHND Sasa yafuata majina ya wana wa Lawi na wazawa wao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa yafuata majina ya wana wa Lawi na wazawa wao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. Neno: Bibilia Takatifu Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). Neno: Maandiko Matakatifu Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. BIBLIA KISWAHILI Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. |
Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, basi umri wake Yakobo ulikuwa miaka mia moja na arubaini na saba.
Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia moja na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Basi Daudi akawagawanya kwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.
Ndipo wakaondoka Walawi, Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa wana wa Wakohathi; na wa wana wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wagershoni, Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa;
Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;
Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari.
Na wana wa Merari kwa jamaa zao ni Mahli, na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kwa nyumba za baba zao.
Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni.
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili.