Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Kutoka 40:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose alitekeleza kikamilifu kabisa maagizo yote ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose alitekeleza kikamilifu kabisa maagizo yote ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose alitekeleza kikamilifu kabisa maagizo yote ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Musa akafanya kila kitu sawa kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akafanya kila kitu sawa kama vile bwana alivyomwagiza. BIBLIA KISWAHILI Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote. |
Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
nawe utawatia mafuta kama ulivyomtia mafuta baba yao, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani; na huko kutiwa mafuta kwao kutakuwa ni kwa ukuhani wa milele katika vizazi vyao vyote.
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi.
Kisha Musa akawaleta wana wa Haruni, na kuwavika kanzu, na kuwafunga mishipi, na kuwavika vilemba; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Kisha akayaosha matumbo na miguu yake kwa maji; na Musa akamteketeza huyo kondoo wote juu ya madhabahu; ilikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza; ilikuwa ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hilo taji takatifu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;