Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 40:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mvike Aroni yale mavazi matakatifu; utampaka mafuta na kumweka wakfu, ili aweze kunitumikia kama kuhani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mvike Aroni yale mavazi matakatifu; utampaka mafuta na kumweka wakfu, ili aweze kunitumikia kama kuhani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mvike Aroni yale mavazi matakatifu; utampaka mafuta na kumweka wakfu, ili aweze kunitumikia kama kuhani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kisha mvike Haruni yale mavazi matakatifu, umpake mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia kama kuhani.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kisha mvike Haruni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 40:13
13 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.


Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kupaka, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.


Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;


Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


Hii ndiyo sehemu ya Haruni, na sehemu ya wanawe, katika kutiwa mafuta kwao, katika hizo dhabihu zisongezwazo kwa BWANA kwa njia ya moto, siku hiyo aliyowaweka ili wamtumikie BWANA katika kazi ya ukuhani;


sehemu ambayo BWANA aliagiza wapewe na wana wa Israeli, siku hiyo aliyowatia mafuta. Ni haki yao ya milele katika vizazi vyao vyote.


Kisha Musa akawaleta wana wa Haruni, na kuwavika kanzu, na kuwafunga mishipi, na kuwavika vilemba; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?


Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.


Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.