Kutoka 40:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Utamwita Aroni na wanawe waje mlangoni mwa hema la mkutano, kisha uwatawadhe. Biblia Habari Njema - BHND “Utamwita Aroni na wanawe waje mlangoni mwa hema la mkutano, kisha uwatawadhe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Utamwita Aroni na wanawe waje mlangoni mwa hema la mkutano, kisha uwatawadhe. Neno: Bibilia Takatifu “Mlete Haruni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. Neno: Maandiko Matakatifu “Mlete Haruni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. BIBLIA KISWAHILI Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji. |
Nawe utawaleta Walawi mbele ya hema ya kukutania; nawe utauitisha mkutano wote wa wana wa Israeli;
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake;
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu zake Aliye Juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,