Ndipo Sipora akashika jiwe gumu lenye makali na kulikata govi ya zunga la mwanawe, na kulibwaga miguuni pa Musa akasema. Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.
Kutoka 4:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi akamwacha. Ndipo huyo mkewe akanena, U bwana arusi wa damu wewe, kwa ajili ya kutahiri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Mwenyezi-Mungu akamwacha Mose. Zipora alikuwa amesema, “Bwana harusi wa damu,” kwa sababu ya kutahiri. Biblia Habari Njema - BHND Hapo Mwenyezi-Mungu akamwacha Mose. Zipora alikuwa amesema, “Bwana harusi wa damu,” kwa sababu ya kutahiri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Mwenyezi-Mungu akamwacha Mose. Zipora alikuwa amesema, “Bwana harusi wa damu,” kwa sababu ya kutahiri. Neno: Bibilia Takatifu (Sipora alipomwita Musa, “Bwana arusi wa damu”, alikuwa anamaanisha ile tohara.) Baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamwacha. Neno: Maandiko Matakatifu Sipora alipomwita Musa, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo bwana akamwacha. BIBLIA KISWAHILI Basi akamwacha. Ndipo huyo mkewe akanena, U bwana harusi wa damu wewe, kwa ajili ya kutahiri. |
Ndipo Sipora akashika jiwe gumu lenye makali na kulikata govi ya zunga la mwanawe, na kulibwaga miguuni pa Musa akasema. Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.
BWANA akamwambia Haruni, Nenda jangwani uonane na Musa. Naye akaenda, akamkuta katika mlima wa Mungu, akambusu.