Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Kutoka 39:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Neno: Bibilia Takatifu Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile bwana alivyokuwa amemwagiza Musa. BIBLIA KISWAHILI Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli. |
Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lolote, wala kwa habari ya hazina.
Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza;
Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.
na mavazi ya kazi nzuri kwa utumishi katika mahali patakatifu, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.
Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.
Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.