Kutoka 36:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi kila mtu mwenye moyo wa hekima miongoni mwa hao waliofanya kazi, akaifanya hiyo maskani ya mapazia kumi; ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu; pamoja na makerubi, kazi ya fundi stadi; ndivyo alivyoyafanya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanaume wote wenye ujuzi walitengeneza hema takatifu kwa mapazia kumi ya kitani safi iliyosokotwa, na kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kuyatarizi viumbe wenye mabawa. Biblia Habari Njema - BHND Wanaume wote wenye ujuzi walitengeneza hema takatifu kwa mapazia kumi ya kitani safi iliyosokotwa, na kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kuyatarizi viumbe wenye mabawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanaume wote wenye ujuzi walitengeneza hema takatifu kwa mapazia kumi ya kitani safi iliyosokotwa, na kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kuyatarizi viumbe wenye mabawa. Neno: Bibilia Takatifu Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani ya Mungu kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. BIBLIA KISWAHILI Basi kila mtu mwenye moyo wa hekima miongoni mwa hao waliofanya kazi, akaifanya hiyo maskani ya mapazia kumi; ya nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu; pamoja na makerubi, kazi ya fundi stadi; ndivyo alivyoyafanya. |
Basi Daudi akajijengea nyumba katika mji wa Daudi; akatayarisha mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema.
Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo lilipokuwako hema la kukutania la Mungu, alilolifanya Musa mtumishi wa BWANA jangwani.
Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akatengeneza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunika kwa dhahabu.
Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza;
yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;
Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza;
Urefu wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa nne; mapazia yote yalikuwa ya kipimo kimoja.
Nao wakaifua hiyo dhahabu hata ikawa mabamba membamba sana, kisha wakaikata iwe nyuzi, ili wapate kuifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyuzi nyekundu na za kitani nzuri, kazi ya fundi stadi sana.