Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 36:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mose alimwita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu ambaye alikuwa amejaliwa ujuzi na Mwenyezi-Mungu, na kila mtu ambaye moyo wake ulimsukuma kufanya kazi kwa hiari.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mose alimwita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu ambaye alikuwa amejaliwa ujuzi na Mwenyezi-Mungu, na kila mtu ambaye moyo wake ulimsukuma kufanya kazi kwa hiari.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mose alimwita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu ambaye alikuwa amejaliwa ujuzi na Mwenyezi-Mungu, na kila mtu ambaye moyo wake ulimsukuma kufanya kazi kwa hiari.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Mwenyezi Mungu alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye bwana alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 36:2
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote; tena maofisa na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.


ya dhahabu, kwa vitu vya dhahabu, na ya fedha kwa vitu vya fedha, na kwa kazi za kila namna zitakazofanywa kwa mikono ya mafundi. Ni nani basi ajitoaye kwa moyo ili ajiweke wakfu leo kwa BWANA?


Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.


Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.


Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.


Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza;


Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza;


Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu yeyote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo atauawa.


Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.


nao wakapokea mkononi mwa Musa matoleo yote, ambayo hao wana wa Israeli walikuwa wameyaleta kwa ajili ya huo utumishi wa mahali patakatifu, ili wapatengeneze. Kisha wakamletea matoleo kila siku asubuhi kwa moyo wa kupenda.


Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.


Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.


Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.