Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Kutoka 36:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Bezaleli na Oholiabu, pamoja na kila mwanamume ambaye Mwenyezi-Mungu amemjalia uwezo na akili ya kujua namna ya kufanya kazi zote katika ujenzi wa hema takatifu, atafanya kazi kulingana na yote ambayo Mwenyezi-Mungu aliamuru.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Bezaleli na Oholiabu, pamoja na kila mwanamume ambaye Mwenyezi-Mungu amemjalia uwezo na akili ya kujua namna ya kufanya kazi zote katika ujenzi wa hema takatifu, atafanya kazi kulingana na yote ambayo Mwenyezi-Mungu aliamuru.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Bezaleli na Oholiabu, pamoja na kila mwanamume ambaye Mwenyezi-Mungu amemjalia uwezo na akili ya kujua namna ya kufanya kazi zote katika ujenzi wa hema takatifu, atafanya kazi kulingana na yote ambayo Mwenyezi-Mungu aliamuru.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu Mwenyezi Mungu aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile Mwenyezi Mungu alivyoagiza.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu bwana aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile bwana alivyoagiza.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Kutoka 36:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.

Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.

Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote; tena maofisa na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.

Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.

Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.

Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.

Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.

na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;

Na pamoja naye alikuwa na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, aliyekuwa fundi wa kuchora nakshi, mfanyaji wa kazi mwerevu, naye alikuwa mwenye kutia taraza za nyuzi za rangi ya samawati, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri.

Na zile nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyatengeneza hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao.

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.

mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.