Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Kutoka 35:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kila mtu mwenye ujuzi wa kazi fulani miongoni mwenu atakuja kufanya vitu vyote alivyoamuru Mwenyezi-Mungu: Biblia Habari Njema - BHND “Kila mtu mwenye ujuzi wa kazi fulani miongoni mwenu atakuja kufanya vitu vyote alivyoamuru Mwenyezi-Mungu: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kila mtu mwenye ujuzi wa kazi fulani miongoni mwenu atakuja kufanya vitu vyote alivyoamuru Mwenyezi-Mungu: Neno: Bibilia Takatifu “Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Mwenyezi Mungu alichoamuru: Neno: Maandiko Matakatifu “Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu bwana alichoamuru: BIBLIA KISWAHILI Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza; |
Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.