wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.
Kutoka 34:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe uwe tayari asubuhi, ukwee juu katika mlima wa Sinai asubuhi, nawe leta nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai. Biblia Habari Njema - BHND Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai. Neno: Bibilia Takatifu Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. Neno: Maandiko Matakatifu Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. BIBLIA KISWAHILI Nawe uwe tayari asubuhi, ukwee juu katika mlima wa Sinai asubuhi, nawe leta nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima. |
wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.
BWANA akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; BWANA akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu.
BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.
BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa vibao vya mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe.
Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.