Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.
Kutoka 33:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu walilia waliposikia habari hizi mbaya; wala hakuna aliyevaa mapambo yake. Biblia Habari Njema - BHND Watu walilia waliposikia habari hizi mbaya; wala hakuna aliyevaa mapambo yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu walilia waliposikia habari hizi mbaya; wala hakuna aliyevaa mapambo yake. Neno: Bibilia Takatifu Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. Neno: Maandiko Matakatifu Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. BIBLIA KISWAHILI Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yake. |
Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.
Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.
Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.
Nami niliposikia hayo, nikararua nguo yangu na joho langu, nikang'oa nywele za kichwa changu, na ndevu zangu, nikaketi kwa mshangao.
Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;
Basi walipoinua macho yao, wakiwa bado kwa mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho lake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.
Tetemekeni, enyi wanawake mnaostarehe; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, na kujivika nguo za magunia viunoni.
Piga kite lakini si kwa sauti ya kusikiwa; usifanye matanga kwa ajili yake yeye aliyekufa; jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usiifunike midomo yako, wala usile chakula cha watu.
Na vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa vyenu, na viatu vyenu miguuni mwenu; hamtaomboleza wala kulia; lakini mtafifia katika maovu yenu, na kusikitika kila mtu pamoja na mwenziwe.
Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika wakitetemeka; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,
Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe Eleazari na Ithamari, Msiache wazi nywele za vichwani mwenu, wala msiyararue mavazi yenu; ili kwamba msife, tena asiukasirikie mkutano wote; lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, na waomboleze kwa ajili ya waliochomwa na moto wa BWANA.
Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
na kusema na makuhani wa nyumba ya BWANA wa majeshi, na hao manabii, ya kwamba, Je! Yanipasa kulia katika mwezi wa tano, na kufunga, kama nilivyofanya miaka hii mingi iliyopita?
Waambie watu wote wa nchi, na hao makuhani, ukisema, Hapo mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na mwezi wa saba, katika miaka hiyo sabini, je, Mlifunga kwa ajili yangu?
Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu elfu hamsini; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu.