Kutoka 33:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akasema, Nakusihi unioneshe utukufu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.” Biblia Habari Njema - BHND Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha Musa akasema, “Basi nioneshe utukufu wako.” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Musa akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.” BIBLIA KISWAHILI Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. |
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyewahi kumwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.