Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Kutoka 32:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, watu wote wakatoa vipuli vyote vya dhahabu masikioni mwao, wakamletea Aroni. Biblia Habari Njema - BHND Basi, watu wote wakatoa vipuli vyote vya dhahabu masikioni mwao, wakamletea Aroni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, watu wote wakatoa vipuli vyote vya dhahabu masikioni mwao, wakamletea Aroni. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Haruni. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Haruni. BIBLIA KISWAHILI Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. |
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.
Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.
Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.
Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya fundi stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawati na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi wao.