Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 32:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Aroni akawajibu, “Chukueni vipuli vya dhahabu masikioni mwa wake zenu, wana wenu na binti zenu, mniletee.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Aroni akawajibu, “Chukueni vipuli vya dhahabu masikioni mwa wake zenu, wana wenu na binti zenu, mniletee.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Aroni akawajibu, “Chukueni vipuli vya dhahabu masikioni mwa wake zenu, wana wenu na binti zenu, mniletee.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Haruni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu, na binti zenu wamevaa, mkaniletee.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Haruni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 32:2
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,


Kisha nikamwuliza, U binti wa nani wewe? Naye akasema, Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia. Nami nikamtia kishaufu puani mwake na vikuku mikononi mwake.


Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.


Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.


Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.


Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.


na pete za masikio, na vikuku, na mataji yao;


Nanyi mtakitia najisi kifuniko cha sanamu zenu za fedha zilizochongwa, na mabamba ya sanamu zenu za dhahabu zilizoyeyushwa; utazitupilia mbali kama kitu kilicho najisi; utasema, Haya, toka hapa.


Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo;


Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye niliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali.