Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 32:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe, ukisema, ‘Nitawazidisha wazawa wenu kama nyota za mbinguni na nchi yote hii niliyowaahidia nitawapa vizazi vyenu wairithi milele.’”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe, ukisema, ‘Nitawazidisha wazawa wenu kama nyota za mbinguni na nchi yote hii niliyowaahidia nitawapa vizazi vyenu wairithi milele.’”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe, ukisema, ‘Nitawazidisha wazawa wenu kama nyota za mbinguni na nchi yote hii niliyowaahidia nitawapa vizazi vyenu wairithi milele.’”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote niliyowaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 32:13
23 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;


BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,


Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.


Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.


Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.


akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,


katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;


BWANA, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atamtuma malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke kutoka huko;


naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.


Itakuwa hapo BWANA atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa,


Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.


BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;


ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.


BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.


bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.


Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie ukaidi wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;


Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,