Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Kutoka 29:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC nawe mvike kile kilemba kichwani, na lile taji takatifu utalitia katika kile kilemba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena utamvika kile kilemba kichwani na kuweka juu ya hicho kilemba ile taji takatifu. Biblia Habari Njema - BHND Tena utamvika kile kilemba kichwani na kuweka juu ya hicho kilemba ile taji takatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena utamvika kile kilemba kichwani na kuweka juu ya hicho kilemba ile taji takatifu. Neno: Bibilia Takatifu Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu lishikamane na hicho kilemba. Neno: Maandiko Matakatifu Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. BIBLIA KISWAHILI nawe mvike kile kilemba kichwani, na lile taji takatifu utalitia katika kile kilemba. |
Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake uko juu yake; mimi ndimi BWANA.
Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hilo taji takatifu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa BWANA akasimama karibu.