Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 29:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho la naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha utachukua yale mavazi ya kikuhani umvike Aroni: Joho, kanzu, kizibao, kifuko cha kifuani, na kumfunga ule mshipi uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha utachukua yale mavazi ya kikuhani umvike Aroni: Joho, kanzu, kizibao, kifuko cha kifuani, na kumfunga ule mshipi uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kisha utachukua yale mavazi ya kikuhani umvike Aroni: joho, kanzu, kizibao, kifuko cha kifuani, na kumfunga ule mshipi uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Chukua yale mavazi na umvike Haruni koti, joho la kizibau, na kizibau chenyewe, pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kizibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Chukua yale mavazi na umvike Haruni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho la naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 29:5
6 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.


Nawe fanya hiyo joho la naivera ya rangi ya buluu yote.


Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wenye kunakishiwa vizuri.


Basi wakaja karibu, na kuwachukua, wakiwa wamevaa nguo zao, wakawachukua nje ya kambi; kama Musa alivyosema.