Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 27:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Vyombo vyote vya hema takatifu vya matumizi ya kila aina, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Vyombo vyote vya hema takatifu vya matumizi ya kila aina, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Vyombo vyote vya hema takatifu vya matumizi ya kila aina, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani ya Mungu kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 27:19
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.


Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba.


Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.


Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.


na vile vigingi vya maskani, vigingi vya ua na kamba zake


Na vigingi vyote vya maskani, na vya ua ulioizunguka pande zote vilikuwa vya shaba.


na vitako vya ua kuuzunguka pande zote, na vitako vya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.


na ukuta wa nguo wa ua, na nguzo zake na vitako vyake, na pazia la lango la ua, na kamba zake, na vigingi vyake, na vyombo vyote vya kutumiwa katika utumishi wa maskani, kwa hiyo hema ya kukutania,


Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.


Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.


Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila kamanda.


na nguzo za ua zilizouzunguka, na vitako yake, na vigingi vyake, na kamba zake.


na viguzo vya ua vya kuuzunguka pande zote, na vitako vyake, na vigingi vyake, na kamba zake, na vyombo vyake vyote, pamoja na utumishi wake wote; nanyi mtawaagizia kila mtu kwa jina lake vile vyombo vya mzigo wao watakaoulinda.