Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.
Kutoka 27:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ua huo utakuwa na urefu wa mita 44, upana wa mita 22, na kimo cha mita 2.25. Vyandarua vyake vitakuwa vya kitani safi na vikalio vyake vya shaba. Biblia Habari Njema - BHND Ua huo utakuwa na urefu wa mita 44, upana wa mita 22, na kimo cha mita 2.25. Vyandarua vyake vitakuwa vya kitani safi na vikalio vyake vya shaba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ua huo utakuwa na urefu wa mita 44, upana wa mita 22, na kimo cha mita 2.25. Vyandarua vyake vitakuwa vya kitani safi na vikalio vyake vya shaba. Neno: Bibilia Takatifu Ua utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. Neno: Maandiko Matakatifu Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. BIBLIA KISWAHILI Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba. |
Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.
Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.
Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.