Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 26:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Pia utatengeneza kifuniko cha hema kwa mapazia kumi na moja ya manyoya ya mbuzi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Pia utatengeneza kifuniko cha hema kwa mapazia kumi na moja ya manyoya ya mbuzi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Pia utatengeneza kifuniko cha hema kwa mapazia kumi na moja ya manyoya ya mbuzi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Maskani.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 26:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu, Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.


na nyuzi rangi za buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi;


Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.


Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani.


Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.


Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganisha hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo; na hiyo maskani itakuwa ni moja.


Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja.


Kisha utaunganisha mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalikunja hapo upande wa mbele wa ile hema.


Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, akavileta.


Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi.


na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi;


Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.


Na kazi ya Wageruhoni katika hema ya kukutania ni hiyo ya kuhudumu katika maskani, Hema na kifuniko chake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania,


Na kuhusu kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe;


wao watayachukua mapazia ya Hema Takatifu, na hema ya kukutania, hizo nguo za kufunikia, na zile ngozi za pomboo za kufunikia zilizo juu yake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania;


bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.