Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.
Kutoka 26:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo utalitengeneza hema hilo kulingana na mfano niliokuonesha mlimani. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo utalitengeneza hema hilo kulingana na mfano niliokuonesha mlimani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo utalitengeneza hema hilo kulingana na mfano niliokuonesha mlimani. Neno: Bibilia Takatifu “Simamisha maskani ya Mungu sawasawa na mfano uliooneshwa kule mlimani. Neno: Maandiko Matakatifu “Simamisha Hema sawasawa na mfano ulioonyeshwa kule mlimani. BIBLIA KISWAHILI Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani. |
Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.
Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.
Na hizo mbao utazifunika dhahabu, na pete zake za kutilia yale mataruma utazifanya za dhahabu; na hayo mataruma utayafunika dhahabu.
Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake; kama ulivyooneshwa mlimani, ndivyo watakavyoifanya.
Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao.
Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu kitako chake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye kulingana na mfano ule aliouona;
mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uliooneshwa katika mlima.
Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.
Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.