Tena ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja.
Kutoka 26:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ile nusu ya pazia iliyobaki utaitundika upande wa nyuma wa hema. Biblia Habari Njema - BHND Ile nusu ya pazia iliyobaki utaitundika upande wa nyuma wa hema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ile nusu ya pazia iliyobaki utaitundika upande wa nyuma wa hema. Neno: Bibilia Takatifu Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia za hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaning’inizwa upande wa nyuma wa maskani ya Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaning’inizwa upande wa nyuma wa Hema. BIBLIA KISWAHILI Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. |
Tena ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja.
Na hiyo dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili, ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika.
Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja.