Kutoka 24:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose akaenda mlimani, na wingu likaufunika mlima. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose akaenda mlimani, na wingu likaufunika mlima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose akaenda mlimani, na wingu likaufunika mlima. Neno: Bibilia Takatifu Musa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, Neno: Maandiko Matakatifu Musa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, BIBLIA KISWAHILI Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. |
Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.
BWANA akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; BWANA akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu.
BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini nawe hata milele. Musa akamwambia BWANA hayo maneno ya watu.
Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.
Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.