Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.
Kutoka 23:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake. Biblia Habari Njema - BHND “Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake. Neno: Bibilia Takatifu “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. Neno: Maandiko Matakatifu “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. BIBLIA KISWAHILI Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. |
Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Ni waasi kupita kiasi wote pia, waendao huku na huko wakisingizia, ni shaba na chuma hao, hutenda dhuluma wote pia.
kama hamwonei mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, wala kuifuata miungu mingine kwa hasara yenu wenyewe;
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.
Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.