Kutoka 23:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini. Biblia Habari Njema - BHND Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini. Neno: Bibilia Takatifu nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. Neno: Maandiko Matakatifu nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. BIBLIA KISWAHILI wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. |
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.