Naye akamwambia maneno yayo hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.
Kutoka 23:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya. Biblia Habari Njema - BHND “Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya. Neno: Bibilia Takatifu “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. Neno: Maandiko Matakatifu “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. BIBLIA KISWAHILI Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. |
Naye akamwambia maneno yayo hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.
Mfalme akasema, Na mwana wa bwana wako yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Angalia, anakaa Yerusalemu; kwani alisema, Leo nyumba ya Israeli watanirudishia ufalme wa babu yangu.
Naye amenisingizia mimi mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako.
Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.
Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.
Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.
Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.
Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
Maana nimesikia shutuma za watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.