naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Kutoka 22:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mtu akiiba ng'ombe au kondoo na kumchinja au kumwuza, atatozwa ng'ombe watano kwa kila ng'ombe, na kondoo wanne kwa kila kondoo. Biblia Habari Njema - BHND “Mtu akiiba ng'ombe au kondoo na kumchinja au kumwuza, atatozwa ng'ombe watano kwa kila ng'ombe, na kondoo wanne kwa kila kondoo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mtu akiiba ng'ombe au kondoo na kumchinja au kumwuza, atatozwa ng'ombe watano kwa kila ng'ombe, na kondoo wanne kwa kila kondoo. Neno: Bibilia Takatifu “Mtu yeyote akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ng’ombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. Neno: Maandiko Matakatifu “Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ng’ombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. BIBLIA KISWAHILI Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. |
naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Au ikiwa ilijulikana ya kuwa ng'ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng'ombe kwa ng'ombe, na huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa ni wake.
Tena katika pindo za nguo zako imeonekana damu ya roho zao maskini wasio na hatia; sikuiona penye mahali palipobomoka, lakini niliiona juu ya hawa wote.
kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang'anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wowote; hakika ataishi, hatakufa.
ndipo watakapoungama dhambi yao waliyoifanya; naye atatoa fidia kwa hatia yake, kwa utimilifu wake, tena ataongeza juu yake sehemu ya tano, na kumpa huyo aliyemkosea.
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.