Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 21:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikiwa aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kama ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama alinunuliwa kabla hajaoa, ataondoka peke yake. Lakini kama alikuja na mkewe, basi, ataondoka na mkewe. Biblia Habari Njema - BHND Kama alinunuliwa kabla hajaoa, ataondoka peke yake. Lakini kama alikuja na mkewe, basi, ataondoka na mkewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama alinunuliwa kabla hajaoa, ataondoka peke yake. Lakini kama alikuja na mkewe, basi, ataondoka na mkewe. Neno: Bibilia Takatifu Akija peke yake, ataenda huru peke yake, lakini akija na mke, ataondoka pamoja naye. Neno: Maandiko Matakatifu Kama akija peke yake, atakwenda huru peke yake, lakini kama akija na mke, ataondoka pamoja naye. BIBLIA KISWAHILI Ikiwa aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kama ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. |
Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Ikiwa ni bwana wake aliyemwoza huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.