Tena ulishuka juu ya mlima Sinai, ukasema nao toka mbinguni, ukawapa hukumu za haki, na sheria za kweli, na amri nzuri na maagizo;
Kutoka 20:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu akanena maneno haya yote akasema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: BIBLIA KISWAHILI Mungu akanena maneno haya yote akasema, |
Tena ulishuka juu ya mlima Sinai, ukasema nao toka mbinguni, ukawapa hukumu za haki, na sheria za kweli, na amri nzuri na maagizo;
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima ili atupe sisi.
Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia BWANA huko mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa.
Je! Kuna wakati wowote watu wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, na wakaendelea kuishi?
Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.
Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.