Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 19:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Makuhani nao, wamkaribiao BWANA, na wajitakase, BWANA asije akawakasirikia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hata makuhani ambao hunikaribia wanapaswa kujitakasa; la sivyo nitawaadhibu.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hata makuhani ambao hunikaribia wanapaswa kujitakasa; la sivyo nitawaadhibu.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hata makuhani ambao hunikaribia wanapaswa kujitakasa; la sivyo nitawaadhibu.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hata makuhani, watakaomkaribia Mwenyezi Mungu ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo Mwenyezi Mungu atawaadhibu.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hata makuhani, watakaomkaribia bwana ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo bwana atawaadhibu.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Makuhani nao, wamkaribiao BWANA, na wajitakase, BWANA asije akawakasirikia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 19:22
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, BWANA, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta kulingana na sheria.


Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA.


Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani wa kutosha walikuwa hawajajitakasa, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.


BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.


Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,


akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng'ombe.


Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.


Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.


Kisha uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa BWANA, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo BWANA atawapa nyama, nanyi mtakula.


Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.


Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.