Tena ulishuka juu ya mlima Sinai, ukasema nao toka mbinguni, ukawapa hukumu za haki, na sheria za kweli, na amri nzuri na maagizo;
Kutoka 19:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sauti ya mbiu ilizidi kuongezeka, na Mose akaongea na Mungu. Mungu naye akamjibu katika ngurumo. Biblia Habari Njema - BHND Sauti ya mbiu ilizidi kuongezeka, na Mose akaongea na Mungu. Mungu naye akamjibu katika ngurumo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sauti ya mbiu ilizidi kuongezeka, na Mose akaongea na Mungu. Mungu naye akamjibu katika ngurumo. Neno: Bibilia Takatifu nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Musa akazungumza, nayo sauti ya Mungu ikamjibu. Neno: Maandiko Matakatifu nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Musa akazungumza na sauti ya bwana ikamjibu. BIBLIA KISWAHILI Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti. |
Tena ulishuka juu ya mlima Sinai, ukasema nao toka mbinguni, ukawapa hukumu za haki, na sheria za kweli, na amri nzuri na maagizo;
Katika shida uliniita nikakuokoa; Nilikuitikia kutoka maficho yangu ya radi; Nilikujaribu penye maji ya Meriba.
Mkono wa mtu yeyote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe, au kupigwa kwa mkuki; awe ni mnyama au awe ni mwanadamu, hataishi. Hapo parapanda itakapotoa sauti kwa kufululiza ndipo watakapoukaribia mlima.
Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.
Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lolote lingine;
Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.