Kutoka 18:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kufanya hivyo, Mose na mkwewe wakaagana naye Yethro akarudi nchini kwake. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kufanya hivyo, Mose na mkwewe wakaagana naye Yethro akarudi nchini kwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kufanya hivyo, Mose na mkwewe wakaagana naye Yethro akarudi nchini kwake. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Musa akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Musa akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake. BIBLIA KISWAHILI Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe. |
Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.
Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria wake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.
Basi akatoka pale alipokuwa akiishi, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda.