Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wazawa wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili.
Kutoka 18:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose alilisikiliza shauri hilo la mkwewe na kufanya kama alivyoshauriwa. Biblia Habari Njema - BHND Mose alilisikiliza shauri hilo la mkwewe na kufanya kama alivyoshauriwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose alilisikiliza shauri hilo la mkwewe na kufanya kama alivyoshauriwa. Neno: Bibilia Takatifu Musa akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. BIBLIA KISWAHILI Basi Musa akalisikiliza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. |
Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wazawa wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili.
Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Waisraeli wote, ya kwamba watafanya hivyo. Basi wakaapa.
Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.
Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi.
mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.