BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Kutoka 17:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose akajenga madhabahu na kuiita, “Mwenyezi-Mungu ni Bendera Yangu”, Biblia Habari Njema - BHND Mose akajenga madhabahu na kuiita, “Mwenyezi-Mungu ni Bendera Yangu”, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose akajenga madhabahu na kuiita, “Mwenyezi-Mungu ni Bendera Yangu”, Neno: Bibilia Takatifu Musa akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi. BIBLIA KISWAHILI Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi; |
BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,
Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa BWANA.
Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.