Neno hili ndilo aliloagiza BWANA, Okoteni ninyi kitu hicho kila mtu kama ulaji wake ulivyo; kila mtu pishi moja kama hesabu ya watu wenu ilivyo; ndivyo mtakavyotwaa, kila mtu kwa ajili ya hao walioko hemani mwake.
Kutoka 16:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hiyo omeri ni sehemu kumi ya efa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema (Posho ya mana, kiasi cha pishi nne, ilikuwa sehemu ya kumi ya kipimo cha kawaida kiitwacho efa.) Biblia Habari Njema - BHND (Posho ya mana, kiasi cha pishi nne, ilikuwa sehemu ya kumi ya kipimo cha kawaida kiitwacho efa.) Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza (Posho ya mana, kiasi cha pishi nne, ilikuwa sehemu ya kumi ya kipimo cha kawaida kiitwacho efa.) Neno: Bibilia Takatifu (Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.) Neno: Maandiko Matakatifu (Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.) BIBLIA KISWAHILI Hiyo omeri ni sehemu kumi ya efa. |
Neno hili ndilo aliloagiza BWANA, Okoteni ninyi kitu hicho kila mtu kama ulaji wake ulivyo; kila mtu pishi moja kama hesabu ya watu wenu ilivyo; ndivyo mtakavyotwaa, kila mtu kwa ajili ya hao walioko hemani mwake.
Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri.
pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa.
Basi Ruthu akaokota mabaki shambani hadi jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri.