Na ulipokauka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama barafu juu ya nchi.
Kutoka 16:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na utamu wake ulikuwa kama utamu wa maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walikiita chakula hicho “Mana.” Kilikuwa kama mbegu za mtama mweupe na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotiwa asali. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walikiita chakula hicho “Mana.” Kilikuwa kama mbegu za mtama mweupe na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotiwa asali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walikiita chakula hicho “Mana.” Kilikuwa kama mbegu za mtama mweupe na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotiwa asali. Neno: Bibilia Takatifu Waisraeli wakaita ile mikate mana. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama, na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. BIBLIA KISWAHILI Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na utamu wake ulikuwa kama utamu wa maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali. |
Na ulipokauka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama barafu juu ya nchi.
Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao BWANA amewapa ninyi, mle.
Musa akasema, Hili ni neno BWANA aliloliamuru, Pishi moja ya kitu hicho na kiwekwe kwa ajili ya vizazi vyenu; ili kwamba wao wapate kukiona kile chakula nilichowalisha ninyi barani, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri.
Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.
aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
Akakunyenyekeza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.