ukawajulisha sabato yako takatifu, na ukawapa maagizo, na amri, na sheria, kwa mkono wa mtumishi wako, Musa.
Kutoka 16:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya BWANA; leo hamtakiona nje barani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mose akawaambia, “Kuleni chakula hicho kilichosalia kwa sababu leo ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu. Leo hamtapata chakula huko nje. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mose akawaambia, “Kuleni chakula hicho kilichosalia kwa sababu leo ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu. Leo hamtapata chakula huko nje. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mose akawaambia, “Kuleni chakula hicho kilichosalia kwa sababu leo ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu. Leo hamtapata chakula huko nje. Neno: Bibilia Takatifu Musa akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa bwana. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. BIBLIA KISWAHILI Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya BWANA; leo hamtakiona nje barani. |
ukawajulisha sabato yako takatifu, na ukawapa maagizo, na amri, na sheria, kwa mkono wa mtumishi wako, Musa.
Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu.
Angalieni, kwa kuwa BWANA amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba.