Kutoka 15:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani; Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani; Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani; Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu ni shujaa wa vita; Mwenyezi Mungu ndilo jina lake. Neno: Maandiko Matakatifu bwana ni shujaa wa vita; bwana ndilo jina lake. BIBLIA KISWAHILI BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. |
Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.
Akayakwamisha magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake ni nani? Niwaambie nini?
Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
BWANA atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.
Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi,