Basi watu hao ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa uweza wako mwingi, na kwa mkono wako hodari.
Kutoka 13:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Adhimisho hilo litakuwa ukumbusho, kama alama katika mikono yenu au katika paji la nyuso zenu; ili iwakumbushe daima sheria ya Mwenyezi-Mungu. Maana, Mwenyezi-Mungu amewatoa nchini Misri kwa mkono wenye nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Adhimisho hilo litakuwa ukumbusho, kama alama katika mikono yenu au katika paji la nyuso zenu; ili iwakumbushe daima sheria ya Mwenyezi-Mungu. Maana, Mwenyezi-Mungu amewatoa nchini Misri kwa mkono wenye nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Adhimisho hilo litakuwa ukumbusho, kama alama katika mikono yenu au katika paji la nyuso zenu; ili iwakumbushe daima sheria ya Mwenyezi-Mungu. Maana, Mwenyezi-Mungu amewatoa nchini Misri kwa mkono wenye nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Mwenyezi Mungu inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Adhimisho hili litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. BIBLIA KISWAHILI Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. |
Basi watu hao ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa uweza wako mwingi, na kwa mkono wako hodari.
Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele
Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri.
Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.
Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa hukumu zilizo kuu.
Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
Nitie kama mhuri moyoni mwako, Kama mhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na fidia yake i mbele zake.
Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Tena kuhusu habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.
Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekung'oa wewe hapo;
Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu.
naye BWANA anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?
nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya; tena ili msiende kutangatanga kufuata mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Lakini yanenaje? Lile neno liko karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.
Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhibika.