Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
Kutoka 13:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utamwambia mwanao siku hiyo, ukisema, Ni kwa sababu ya hayo BWANA aliyonifanyia hapo nilipotoka Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo mtawaambia watoto wenu kwamba mnafanya hivyo kwa sababu ya jambo alilowafanyia Mwenyezi-Mungu mlipoondoka nchini Misri. Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo mtawaambia watoto wenu kwamba mnafanya hivyo kwa sababu ya jambo alilowafanyia Mwenyezi-Mungu mlipoondoka nchini Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo mtawaambia watoto wenu kwamba mnafanya hivyo kwa sababu ya jambo alilowafanyia Mwenyezi-Mungu mlipoondoka nchini Misri. Neno: Bibilia Takatifu Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Mwenyezi Mungu alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ Neno: Maandiko Matakatifu Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ BIBLIA KISWAHILI Nawe utamwambia mwanao siku hiyo, ukisema, Ni kwa sababu ya hayo BWANA aliyonifanyia hapo nilipotoka Misri. |
Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.
Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, Ni nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?