Nao wana wa Israeli waliokusanyika Yerusalemu wakafanya sikukuu ya mikate isiyochachwa siku saba kwa furaha kubwa; Walawi na makuhani wakamsifu BWANA siku kwa siku, wakimwimbia BWANA kwa vinanda vyenye sauti kuu.
Kutoka 13:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba, nayo siku ya saba itakuwa ni sikukuu ya BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, na mnamo siku ya saba mtafanya sikukuu kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, na mnamo siku ya saba mtafanya sikukuu kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, na mnamo siku ya saba mtafanya sikukuu kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Mwenyezi Mungu sikukuu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia bwana sikukuu. BIBLIA KISWAHILI Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba, nayo siku ya saba itakuwa ni sikukuu ya BWANA. |
Nao wana wa Israeli waliokusanyika Yerusalemu wakafanya sikukuu ya mikate isiyochachwa siku saba kwa furaha kubwa; Walawi na makuhani wakamsifu BWANA siku kwa siku, wakimwimbia BWANA kwa vinanda vyenye sauti kuu.
Hiyo sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu utaitunza. Utakula mikate isiyotiwa chachu muda wa siku saba, kama nilivyokuagiza, kwa majira yaliyoaganwa katika mwezi wa Abibu; kwa kuwa ulitoka Misri katika mwezi huo wa Abibu.
Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.
Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa BWANA, Mungu wako, usifanye kazi yoyote.
Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya Pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo.