Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje kondoo wa Pasaka.
Kutoka 13:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; na kama hutaki kumkomboa, utamwua; na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mzaliwa wa kwanza wa kiume wa punda utamkomboa kwa kulipa mwanakondoo, la sivyo, utamuua kwa kumvunja shingo. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa binadamu utamkomboa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mzaliwa wa kwanza wa kiume wa punda utamkomboa kwa kulipa mwanakondoo, la sivyo, utamuua kwa kumvunja shingo. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa binadamu utamkomboa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mzaliwa wa kwanza wa kiume wa punda utamkomboa kwa kulipa mwanakondoo, la sivyo, utamuua kwa kumvunja shingo. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa binadamu utamkomboa. Neno: Bibilia Takatifu Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hutamkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa. BIBLIA KISWAHILI Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; na kama hutaki kumkomboa, utamwua; na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. |
Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje kondoo wa Pasaka.
Waambieni mkutano wote, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena ikiwa hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hakuna atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.
Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.