Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
Kutoka 1:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote. Biblia Habari Njema - BHND Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote. Neno: Bibilia Takatifu Basi Yusufu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, Neno: Maandiko Matakatifu Basi Yusufu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, BIBLIA KISWAHILI Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. |
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia moja na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.