Kutoka 1:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.” Biblia Habari Njema - BHND “Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.” Neno: Bibilia Takatifu “Mtakapowazalisha wanawake Waebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni; lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” Neno: Maandiko Matakatifu “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” BIBLIA KISWAHILI akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi. |
Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;
Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake wote, akisema, Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.
Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.
Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme.
Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake.